Ads 468x60px

Featured Posts

Thursday, July 18, 2013

ICC, MASHAHIDI WATATU WAONDOLEWA KESI YA KENYATTA


Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, Bi. Fatou Bensouda, ameondoa mashahidi watatu kwenye kesi ya jinai dhidi ya binadamu inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Bensouda amesema mashahidi wawili wamesema kwamba hawawezi kuendelea kuwa mashahidi kwenye kesi hiyo kutokana na kuhofia usalama wao,pi ametathmini ushahidi wa shahidi mwingine na ameona hauna umuhimu mkubwa na  kuamua kumuondoa.
Mahakama ya ICC majuma kadhaa yaliyopita iliamua kwamba, Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto atahudhuria vikao muhimu tu vya kesi yake mjini Hague na kisha kushiriki  vikao vya kawaida kwa njia ya video.
Wachambuzi wa masuala ya kisheria wanasema hatua hiyo ina maanisha kwamba kesi dhidi ya Rais Kenyatta na Makamu wake zinaendelea kuwa dhaifu na huenda wakafutiwa mashtaka iwapo matukio kama hayo yataendelea kushuhudiwa.


Saturday, July 13, 2013

Saudia yawaonya mahujaji kuhusi hatariu kirusi hatari

                                                                 
Wizara ya Afya nchini Saudi Arabia imetoa onyo kwa Mahujaji na kuwataka wavae (mask) katika maeneo yenye misongamano mikubwa ili kuzuia kuenea kirusi hatari.( Kirusi hicho kinashabihiana na kile cha SARS ambacho kiliua karibu watu 800 mwaka 2003.)

Katika taarifa yake Wizara ya Afya Saudi Arabia imetoa orodha ya masharti kwa mahujaji wanaopanga kutembelea maeneo matakatifu nchini humo ili kuzuia kirusi kijulikanacho kama Middle East Respiratory Syndrome coronavirus (MERS-CoV). Taarifa hiyo imewataka wazee na wale wenye magonjwa sugu kuakhirisha safari za Hijja au Umra.

Hadi sasa watu 38 wamepoteza maisha nchini Saudi Arabia kutokana na kirusi hicho hatari. Maafisa wa afya wa Saudi wamewataka watu wote wadumishe usafi binafsi katika maeneo ya umma, watumie kikaratasi au kitambaa wanapopiga chafya au kukohoa na wawe na chanjo zote zinazohitajika.

Msimu wa Hija mwaka huu utaangukia Mwezi Oktoba, pamoja na hayo Waislamu hufanya ziara katika miji mitakatifu ya Makka na Madina katika kipindi chote cha mwaka. Kirusi cha MERS-CoV kiliibuka mara ya kwanza nchini Saudi Arabia Septemba mwaka 2012 na kimesharipotiwa Jordan, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Tunisia na Uingereza.

Friday, July 12, 2013

HALMASHAURI YA BABATI YAFUTA LESENI ZA BIASHARA



http://www.mwankama.com/images/Babati.gifHalmashauri ya Wilaya ya Babati vijijini, Mkoani Manyara imefuta rasmi leseni zote za biashara zilizokatwa kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 kabla ya muda halisi wa mwisho wa kutumika kwa leseni hizo mwezi julai mwaka huu.

Kwa mujibu wa agizo hilo lililotolewa na Mkurugenzi wa Wilaya ya Babati vijijini Dominic Kweka katika kata ya Bashnet, leseni zote za biashara zilizoishia juni 30 mwaka huuzinatakiwa zikatwe upya kwa ajili ya matumizi ya kuendeshea biashara husika.

Kweka amesema kuwa kila mfanyabiashara anatakiwa kukata upya leseni yake na mwisho wa zoezi hilo ni julai 8 mwaka huu na kuanzia Julai 9 wafanyabiashara watakaokaidi agizo hilo watakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Aidha ameeleza kwamba uamuzi huo umetokana na mabadiliko ya bajeti ya Serikali kwani awali ilikuwa ikisomwa kila mwezi juni na mwaka huu imekuwa tofauti ambapo ilisomwa mwezi April, hivyo kubadili mfumo wa ubadilishwaji wa leseni hizo.

Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara katika kata hiyo wamedai kwamba Serikali haikuwatendea haki kwani kabla ya kutoa matangazo hayo ingekaa na nao na kuwaelimisha juu ya jambo hilo.

WAFUNGWA 200 WATOROKA JAKARTA



Wafungwa 200 wametoroka baada ya fujo kutokea katika gereza lenye wafungwa wengi katika eneo la Medan kaskazini mwa Sumatra mjini Jakarta, Indonesia. 
 http://images.smh.com.au/2013/07/12/4564978/prison-w-620x349.jpg
Habari zinasema wafungwa hao walianza fujo baada ya maji na umeme kukatika katika gereza hilo la Tanjung Gusta. 

Wafungwa hao wanadaiwa kuvunja mlango mkuu wa gereza hilo na kudhibiti sehemu ya gereza hilo huku wakipambana na vikosi vya usalama.

DAWATI LA HABARI TRIPLE A TANZANIA

SIKU ZOTE USHIRIKIANO NI KITU CCHA MUHIMU KATIKA NYANJA YOYOTE ILE, KWA MAENDELEO.
 KUTOKA KUSHOTO NICE STANSLUS,NATORIVOKI LOISHIYE, JOHNSON JABIR, TABITHA HUDSON NA AMIR MONGI KATIKA DAWATI LA HABARI LA TRIPLE A ARUSHA-TANZANIA
UTANI WAKATI MWINGINE UPO UNAPOZIDI KARIPIO LAZIMAAAA!
WA KWANZA KUSHOTO NI GASPER MAKUNGU
 

TABITHA HUDSON, NICE STANSLAUS NA NATORIVOKI KATIKA POZI

 TABITHA HUDSON

 NICE STANLAUS NA NATORIVOKI
 NICE STANLAUS
 TABITHA HUDSON NA NATORIVOKI
NICE STANLAUS, TABITHA HUDSON NA NATORIVOKI LOISHIYE (MWENYE MAJI YA BAHARI)
  WADAU WA KUTOSHA KILA PEMBE YA DUNIA SASA WADAU HAWA WAKO JIJINI ARUSHA TANZANIA KATIKA POZI LA UKUMBUSHO KATIKA TRIPLE A RADIO 

Thursday, July 11, 2013

CHISSANO NA MBEKI KUFUATILIA MGOGORO WA ZIWA NYASA

Chissano, Mbeki, kufuatilia mgogoro wa Ziwa Nyasa Marais wa zamani wa Msumbiji na Afrika Kusini wanatarajiwa kuelekea nchini Malawi siku ya Jumapili ili kuzungumza na viongozi wa nchi hiyo kuhusu mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Malawi na Tanzania.

Joachim Chissano na Thabo Mbeki watafanya mazungumzo na Rais Joyce Banda, Waziri wa Mambo ya Nje na maafisa wengine wa ngazi za juu wa Malawi kabla ya kuelekea Tanzania kwa mazungumzo kama hayo. Tanzania na Malawi zimekuwa zikivutana kuhusu mpaka wa Ziwa Nyasa ambapo Malawi inadai mpaka wake na Tanzania upo katika ufukwe huku Tanzania ikidai kwamba mpaka uko katikati ya ziwa. Hii ni Mara ya kwanza kwa Chissano na Mbeki kufuatilia rasmi kadhia hiyo tangu iwasilishwe kwenye jukwaa la marais wastaafu wa Jumuiya ya SADC mwaka huu.

WATU 15 WAPOTEZA MAISHA KENYA

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/0a25dffd6865b819330e7418c136a45a_XL.jpgWatu wasiopungua 15 wakiwemo wanafunzi wa shule wamepoteza maisha huko Kenya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka Jana jioni katika kaunti ya Kisii, magharibi mwa nchi hiyo.

Afisa mkuu wa polisi katika eneo la Gucha, Mark Ondego amesema mashuhuda wanasema kuwa basi hilo lilipoteza mwelekeo na kupinduka mara kadhaa. Kati ya watu walio poteza maisha nipamoja na dereva wa basi, wanafunzi na waalimu ambao walikuwa wakielekea katika eneo la Nyamache kwa ajili ya michezo ya shule.

Rais Uhuru Kenyatta ametuma salamu za rambi rambi kwa walio ondokewa na ndugu na jamaa zao na kutoa pole kwa majeruhi wa ajali hiyo . . Aidha Rais Kenyatta ameamurumajeruhi  wasafirishwe kwa ndege kutoka Kisii hadi Nairobi kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatt

CAIRO


Mwendesha mashtaka mkuu wa Misri, ameagiza kukamatwa kwa kiongozi mkuu wa kundi la Muslim Brotherhood Mohammed Badie ambapo analaumiwa kwa kuchochea ghasia zilizotokea mjini Cairo ambapo watu 51 waliuawa. 

Amri ya kuwakamata viongozi wengine wapatao 100 wa kundi la Brotherhood imetolewa na baadhi wamewekwa kizuizini ambapa agizo hilo linajiri wakati Waziri Mkuu mteule yuko mbioni kuteua serikali mpya baada ya kuondolewa madarakani kwa Mohammed Morsi.
 
Chama cha kisiasa cha  Freedom and Justice Party kimesema hakitajiunga na utawala wa mpito na kimekataa wadhifa wa uwaziri kilichotengewa na Waziri MKuu Hazem al-Beblawi.

Msemaji wa Muslim Brotherhood Gehad El- Haddad ameambia vyombo vya habari kwamba amri ya kumkamata Badie ni njama za jeshi kuzima maandamano na kulaumu jeshi kwa kuwafyatulia risasi waandamanaji wakati wakifanya maombi nje ya kambi kuu ya jeshi.

Kwa upande wake, jeshi limesema lilikua likijibu shambulio kutoka kwa waandamanaji waliokuwa na silaha.

Wednesday, July 10, 2013

BOKO HARAM WAHUKUMIWA KIFUNGO JELA NIGERIA

Mahakama moja ya Nigeria imewahukumu kifungo cha maisha jela wanachama wanne wa kundi la Boko Haram kwa kuhusika katika mashambulizi matatu makubwa ambapo walitumia mada za miripuko za viwandani karibu na Abuja mwaka 2011.
http://static.guim.co.uk/sys-images/Guardian/Pix/pictures/2013/5/9/1368128242338/Members-of-the-Boko-Haram-010.jpg
Mbali na hao wanne, mwanachama mwingine wa tano wa Boko Haram amehukumiwa kifungo cha miaka kumi jela na wa sita ameachiwa huru kwa kukosekana ushahidi.

Kundi la Boko Haram linadai kuwa mfumo wa Magharibi wa elimu ni haramu na linafanya mashambulizi yake dhidi ya kila mtu anayepinga fikra hiyo.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa, hadi kufikia sasa zaidi ya watu elfu tatu wameuliwa na na kundi la Boko Haram huko Nigeria, mashambulizi ya karibuni kabisa yakiwa ni yale yaliyofanywa na kundi hilo kwenye shule moja ya jimbo la Yobe la kaskazini mwa Nigeria na kupelekea kuuawa wanafunzi 41 na mwalimu mmoja.

Gavana wa jimbo hilo la la Yobe la kaskazini mwa Nigeria ametoa amri ya kufungwa shule zote za sekondari katika jimbo hilo hadi mwezi Septemba, ili kuepusha mashambulio zaidi ya kundi la Boko Haram kwenye shule za jimbo hilo.

MARANGU




MARANGU
KUFUATIA tukio la moto lililotokea katika hifadhi ya msitu wa mlima Kilimanjaro Julai saba mwaka huu kushika kasi katika maeneo ya Rombo na Kilema, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas  Gama ameziagiza Wilaya zote za mkoa huo, kutoa askari mgambo  walioko katika wilaya zao  kushiriki operesheni maalum  ya kuzima moto huo.
Tayari watu zaidi ya 200 wakiwemo  askari walioko kwenye mafunzo katika Chuo Cha Polisi Moshi wameendelea kushirikiana kuuzima moto huo ambao mpaka sasa wamefanikiwa kudhibitii moto huo  kwa asilimia 75.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea neo hilo Meneja mahusiano kutoka hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete  alisema moto huo ulioanza siku ya jumapili julai saba umeendelea kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa bila kuathiri shughuli zozote za utalii katika hifadhi ya mlima.

Alisema moto huo ambao sasa unawaka  katika maeneo mawili tofauti ikiwemo eneo la Rombo  na  Kilema juu  imewalazimu kuweka kambi mbili tofauti  ambapo kambi ya moja imewekwa  eneo la Marangu  kwa wanaozima msitu uliopo Kilema juu  huku kambi nyingine ikiwa imewekwa Rombo kwa wale wanaozima maeneo ya Rombo.

Alisema moto huo umeathiri zaidi maeneo ya Amboni,Ushiri,Keryo,Kimori na Shimbi na kwamba kwa sasa jitihada zinafanyika kuhakikisha moto huo unakwisha  na kwamba mpaka sasa taarifa za awali zinaonyesha chanzo cha moto huo ni watu waliokua wakirina asali kiholela waliwasha moto katikati ya m situ.

Alisema licha ya moto huo kuwa mkubwa na kuunguza zaidi ya hekari 40 haujaathiri shughuli zozote za kitalii zinazoendelea katika hifadhi ya mlima huo na kwamba shughuli zote za kitalii zinaendelea kama kawaida.

Alisema hifadhi ya Taifa kwa kushirikiana na jeshi la polisi wanaendelea na juhudi za kutafuta waliohusika na uharibifu huo na mara zoezi  la kuuzima moto litakapokamilika taarifa ya tathmini ya madhara ya moto itafanywa.

Hii ni mara ya pili moto mkubwa kuwaka katika eneo hilo hilo ambapo moto kama huo uliwaka mwaka 2009 na kusababisha hasara kubwa  kwa misitu na viumbe hai.